Kiwanda cha Sukari Kuanzishwa Tarime
WAKAZI wa vijiji vinavyozunguka bonde la mto Mara, Bisarye, Rwegita, Matongo na Bukenye, wilayani Tarime, mkoani Mara, wametakiwa kuwekeza katika kilimo cha miwa kufuatia ujio wa kiwanda kinachozalisha sukari kujengwa katika maeneo hayo baada ya Sikukuu ya Pasaka.
Akizungumza katika kikao maalumu cha wadau wa maendeleo mbalimbali ya mkoa huo, Mkuu wa wilaya ya Tarime, Glorious Luoga, alisema uongozi wa wilaya hiyo umebaini uwapo wa bonde la mto huo, ni kichocheo kikubwa katika kilimo cha miwa na kutafuta wawekezaji wa kiwanda cha sukari.
“Tuliamua kutafuta wawekezaji na tukawapata ambao ni kampuni ya Nile Agro Industries limited, kutoka nchini Uganda, tulikubaliana nao na tukatembelea viwanda vitatu vinavyozalisha sukari nchi jirani ya Kenya eneo la Migori ili kujifunza na kuona uendeshwaji wa kiwanda cha sukari unavyofanyika,” alisema.
Alisema wawekezaji wanatarajia kuweka shamba la miwa lenye heka 4,439 kwa wakati mmoja pia mashamba madogo ya wananchi yenye heka 1,297 na kutarajiwa kuzalisha miwa 5,000 kwa siku. Aidha zaidi ya watu 5,000 kupata ajira na kutengeneza sukari tani zipatazo 450 kwa siku.
‘’Mgodi wa Acacia umetuahidi mbolea kwa mwaka mmoja tunataka tubadilishe wilaya yetu ya Tarime kutoka kwenye chanzo kimoja cha mapato (mgodi North Mara), kwenda katika kilimo cha miwa na kazi hii inatarajiwa kuanza baada ya Pasaka,” alisema.
Mkuu wa mkoa huo, Charles Mlingwa, alisema harakati hizo zinafanyika ili kutimiza agizo la Rais John Magufuli la uchumi wa viwanda nchini.
Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya wilaya hiyo, Apoo Tindwa, alisema wilaya hiyo ina kiwanda kimoja cha chai na kinasuasua kwa kuzingatia hilo amewataka wawekezaji wengine kuwekeza katika shughuli nyingine za miradi ya maendeleo zilizopo wilayani hapo.

Hakuna maoni: