VYAKULA VYA MAMA MZAZI
Vyakula vya Mama Mzazi
Kuna baadhi ya akina mama wanapotoka kujifungua katika kipindi kile muhimu cha kunyonyesha huwa maziwa yanakuwa kidogo sana kiasi cha kutomtosheleza mtoto
Tatizo hili ni baya kwa sababu mtoto anapozaliwa anahitaji sana kupata maziwa ya mama ya kutosha kwa muda usiopungua miezi 6
Maziwa ya mama yana lishe zote zinazohitajika kwa mtoto na kama mtoto huyu atapata maziwa ya kutosha basi bila shaka atakuwa ni mwenye afya njema na watoto wanaopata maziwa kidogo afya zao huwa si njema sana.
JINSI YA KUONDOA TATIZO HILI
Kuna njia nyingi za asili katika kuondoa hili tatizo,lakini kwa leo ntazungumzia njia chache tuu ambazo ni muhimu zaidi na ndizo zinazojaza haraka maziwa kifuani kwa mama mwenye mtoto mchanga
SUPU YA NG'OMBE,MBUZI NA KONDOO
Mwanamama anapotoka kujifungua ni vizuri apate supu kila asubuhi na ni vizuri zaidi akapata supu ya kongoro,nyama ya ngombe au supu ya kondoo kwani supu za namna hii ni tiba nzuri kwa mama mwenye matatizo ya kutopata maziwa ya kutosha kwa ajili ya mtoto wake na pia hurejesha nguvu zilizopotea wakati wa mshikemshike wa kujifungua.
NDIZI ZA KUCHEMSHA
Pia ndizi za kuchemsha ni nzuri sana kwa kuondoa hili tatizo la kukosa maziwa kwa mama mjamzito,zichemshwe vya kutosha mpaka ziwe laini na hata mtori pia unafaa katika kutibu hali hyo.
MAJI
Mzazi anapaswa awe ni mwenye kujitahidi kunywa maji ya kutosha kila siku kwani nayo humsaidia kuongeza maziwa kwa ajili ya mwanae mpya,pia mzazi kukandwamaji ya moto sehemu za siri si chini ya wiki moja ni vizuri zaidi kwani humsaidia kupata nguvu na kuufanya uke hurudi katika hali ya kawaida kwa muda mfupi.
UJI WA PILIPILI MTAMA
Aidha mzazi anashauriuwa anywe uji wenye pilipili mtama na sio pilipili hizi za chachandu,kwani pilipili mtama zina faida mbili kwa mzazi1.huondoa haraka makovu yaliyotokana na msuguano wa mtoto tumboni
2.husaidia ongezeko la maziwa ya mama ili yapatikane ya kutosha kuweza kumnyonyesha mwanae na akapata afya njema
Hakuna maoni: