MWENDESHA BODABODA AFARIKI DUNIA KWA KUGONGWA NA GARI AKIMKIMBIA ASKARI POLISI.
Kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga ACP Muliro Jumanne Muliro
*****
Kijana aliyejulikana kwa jina la Boazi William mkazi wa kata ya Ndembezi mjini Shinyanga amefariki dunia kwa kugongwa gari wakati akimkimbia askari polisi.
Inaelezwa kuwa kijana huyo amefariki dunia leo mchana wakati akijaribu kumkimbia askari wa usalama barabarani aliyemtaka asimame kutokana na makosa ya barabarani.
Askari anayedaiwa kusababisha kifo hicho ni miongoni mwa askari ambao wamekuwa wakitapakaa mjini Shinyanga wakiwa na fimbo kisha kukamata waendesha bodaboda.
Kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga ACP Muliro Jumanne Muliro amewasihi waendesha bodaboda kutofanya vurugu kwani jambo hilo analishughulikia na atatoa taarifa.
Taarifa zaidi tutawaletea hivi punde
Hakuna maoni: